• HABARI MPYA

    Friday, July 21, 2017

    RATIBA LA LIGA YATOKA, REAL NA BARCA DESEMBA 20 BERNABEU

    Lionel Messi ataiongoza Barcelona kumenyana na Real Madrid ya Cristiano Ronaldo Desemba 20 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


    MECHI ZA UFUNGUZI LA LIGA MSIMU MPYA 

    Sevilla vs Espanyol
    Malaga vs Eibar
    Celta Vigo vs Real Sociedad
    Valencia vs Las Palmas
    Barcelona vs Real Betis
    Deportivo La Coruna vs Real Madrid
    Leganes vs Alaves
    Villarreal vs Levante
    Atletico Madrid vs Girona
    Athletic Bilbao vs Getafe 
    MAHASIMU Real Madrid na Barcelona watamenyana Desemba 20 katika mchezo wa kwanza El Clasico msimu wa 2017-2018 kwa mujibu 3a ratiba ya La Liga iliyotoka leo.
    Mashabiki wa soka Hispania watashuhudia mchezo huo mkali Uwanja wa Santiago Bernabeu hiyo ikiwa ni futrsa ya kwanza ya msimu kushuhudia mwendelezo wa upinzani wa wanasoka wawili wakubwa, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo uwanjani.
    Tarehe ya El Clasico ya kwanza msimu huu inaweza kuwa tatizo kwa Madrid, ambao wataingia kwenye mchezo siku nne baada ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA mjini Abu Dhabi, Desemba 16.
    Mchezo wa marudiano utafanyika Uwanja wa Nou Camp Mei 6, wikiendi ya tatu ya kuelekea mwisho wa msimu na unatarajiwa kuwa wa kuamia mbio za ubingwa, Barcelona wakitarajiwa kujipanga kuipokonya ubingwa Real Madrid.

    Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya Real Madrid kutwaa taji la La Liga kufuatia ushindi dhidi ya Malaga PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    MECHI MUHIMU ZA LA LIKA MSIMU MPYA

    Atletico Madrid vs Real - Novemba 19
    Real Madrid vs Barcelona - Desemba 20 
    Real Madrid vs Atletico - Aprili 9
    Barcelona vs Atletico - Mei 6 
    Mechi ya kwanza ya mahasimu wa Madrid katika Uwanja mpya wa Atletico, Wanda Metropolitano inatarajiwa kufanyika Novemba 19 katika moja ya mechi mbili za kuwakutanisha wapinzani hao, huku mechi ya marudiano ikitarajiwa kupigwa Aprili 8 mwakani Uwanja wa Bernabeu.
    Real Madrid wanatarajiwa kuanza kampeni yao ya kutetea taji la La Liga kwa kumenyana na Deportivo La Coruna wakati Barcelona wataanzia na nyumbani dhidi ya Real Betis.  
    Atletico walitarajiwa kucheza mechi yao ya kwanza ya msimu mpya katika Uwanja wao mpya, Wanda Metropolitano lakini sasa wataanzia ugenini dhidi ya Girona wakati matengenezo ya uwanja wao yakikamilika. 
    clash on July 29 before a two-legged Spanish Super Cup tie in August. 

    Lionel Messi alifunga bao la ushindi la kukumbuk3wa dhidi ya Real Madrid April PICHA ZAIDI GONGA HAPA  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RATIBA LA LIGA YATOKA, REAL NA BARCA DESEMBA 20 BERNABEU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top