• HABARI MPYA

  Wednesday, July 19, 2017

  NEYMAR AKUBALI KUTUA PSG KWA PAUNI MILIONI 195

  MSHAMBULIAJI Neymar amekubali ofa ya Paris Saint-Germain kumuhitaji kwa dau la Pauni Milioni 195, kwa mujibu wa taarifa nchini Brazil.  
  Chaneli ya micheo ya Brazil, Esporte Interativo imeripoti kwamba nyota huyo wa Barcelona amekubaliana vipengele vya mkataba na PSG kuelekea uhamisho wa rekodi kubwa ya dunia, Pauni Milioni 195.
  PSG imejibu taarifa hizo kwa kuliambia gazeti la L’Equipe jana kwamba ni kweli wanamtaka Neymar, lakini hawajatoa ofa iliyotajwa.
  Mapema Jumatatu, gazeti la michezo Barcelona, Sport liliripoti likiwanukuu watu wa karibu wa Mbrazil huyo kwamba ‘hana furaha’ katika klabu hiyo, kwa sababu anabaki kwenye kivuli cha akina Leo Messi na na Luis Suarez.
  Neymar amekubali kuhamia Paris Saint-Germain kwa ada ya Pauni Milioni 195 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

  Barcelona nayo inamtaka kiungo Mtaliano wa PSG, Marco Veratti ambaye dau lake ni Pauni Milioni 88. 
  Kiungo huyo anaweza kufanywa sehemu ya dili ya Neymar kwa maana ya kwamba, PSG wanaweza kutoa Pauni Milioni 108 tu kutimiza ndoto za muda mrefu za Rais Nasser Al-Khelaïf kuwa na wachezaji watatu wakubwa wa kiwango cha kidunia katika klabu.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR AKUBALI KUTUA PSG KWA PAUNI MILIONI 195 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top