• HABARI MPYA

  Thursday, July 20, 2017

  YANGA YASAJILI WINGA ALIYEKATAA URAIA WA UGANDA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imemsajili kiungo chipukizi, Baruan Yahya Akilimali aliyekuwa anasoma nchini Uganda kwa mkataba wa miaka miwili.
  Winga huyo wa kulia anayeweza kucheza na upande wa kushoto pia, amesaini leo mkataba wa miaka miwili kujiunga na wana Jangwani hao.
  Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba wamekuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu mchezaji huyo kabla ya kuridhishwa naye na kuamua kumsajili.
  Baruan Yahya Akilimali aliyekuwa anasoma nchini Uganda amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Yanga

  Baada ya kuonyesha kipaji kikubwa katika mashindano ya shule za sekondari Uganda mwaka juzi, mdogo huyo wa winga wa zamani wa Simba, Akilimali Yahya alishawishiwa kuchukua uraia wa nchi hiyo ili achezee timu ya vijana ya taifa hilo, The Kobs, lakini akakataa.
  Yanga wanaamini huyo ndiye mrithi haswa wa winga wao machachari, Simon Happygod Msuva aliye mbioni kujiunga na timu ya Ligi Kuu nchini Morocco, Difaa Hassani El-Jadida, ambayo inamchukua yeye na Mtanzania mwingine, winga pia Ramadhani Singano ‘Messi’ kutoka Azam FC.
  Timu hiyo yenye maskani yake mji wa El Jadida ikiwa inatumia Uwanja wa El Abdi inataka kujaribu kutwaa taji la Ligi Kuu ya Morocco, inayojulikana kama Botola, moja ya Ligi bora kabisa barani Afrika.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASAJILI WINGA ALIYEKATAA URAIA WA UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top