• HABARI MPYA

    Monday, July 03, 2017

    ARSENAL YAAFIKI KUTOA PAUNI MILIONI 44 KUMSAJILI LACAZETTE

    KLABU ya Arsenal imekubaliana na Lyon kumsajili mshambulaji Mfaransa, Alexandre Lacazette kwa dau ambalo linaweza kuwa la rekodi, Pauni Milioni 44.
    Dili hilo litavunja rekodi ya usajili wa Pauni Milioni 42.5 ambazo Arsenal ilitumia kumsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid mwaka 2013 na inatarajiwa kukamilisha uhamisho wake ndani ya saa 48 zijazo, baada ya Lacazette kusafiri kwenda London kwa vipimo.
    Arsenal ilijaribu bila mafanikio kutuma ofa ya Pauni Milioni 29 kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwaka mmoja uliopita na sasa imepandisha dau hadi Pauni Milioni 39.5 ambazo awali zilikataliwa kabla ya kufikia makubaliano na mmiliki wa Lyon, Jean-Michel Aulas.
    Alexandre Lacazette (kulia) amekwenda London kufanya vipimo vya afya tayari kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Arsenal, Pauni Milioni 44 

    Lacazette amekuwa na Lyon tangu anaanza soka yake ya ushindani akiigungia mabao 129 katika mechi 275 timu hiyo ya nyumbani kwao. Msimu uliopita alifunga mabao 37 katika mechi 45. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YAAFIKI KUTOA PAUNI MILIONI 44 KUMSAJILI LACAZETTE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top