• HABARI MPYA

    Saturday, July 22, 2017

    ALVARO MORATA TAYARI NI MCHEZAJI WA CHELSEA YA ENGLAND

    Alvaro Morata akiwa ameshika jezi ya Chelsea baada ya kukamilisha uhamisho wake leo kutoka Real Madrid PICHA ZAIDI GONGA HAPA  


    MABAO YA MORATA KATIKA LA LIGA 

    Jumla ya dakika alizocheza: 1,331 
    Mabao: 15
    Pasi za mabao: 4
    Dakika kwa bao: 89
    Shuti kwa bao: 3.6
    )Takwimu hizo ni kwa msimu uliopita wa 2016-17 wa La Liga) 
    KLABU ya Chelsea imekamilisha uhamisho wa Alvaro Morata kutoka Real Madrid kwa ada ya Pauni Milioni 70.6.
    Mshambuliaji huyo wa Hispania aliwasili Uwanja wa Ndege wa Heathrow Alhamisi, na The Blues sasa imethibitisha usajili huo wa dau la rekodi la klabu baada ya mchezaji huyo kupasi vipimo vya afya Cobham.
    Morata amesaini mkataba wa miaka mitano Stamford Bridge, ambao utafanya awe analipwa kiasi cha Pauni 155,000 kwa wiki na ataungana na wachezaji wengine wa kikosi cha Chelsea mjini Singapore wiki ijayo.
    Baada ya kukamilisha huo, Morata alisema: "Nina furaha sana kuwa hapa. Ni sifa kubwa kuwa sehemu ya klabu hii. Naangalia namna ya kufanya kazi kwa bidii, kufunga mabao mengi niwezavyo na kushinda mataji mengi,". 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALVARO MORATA TAYARI NI MCHEZAJI WA CHELSEA YA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top