• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2016

  SIMBA NA YANGA ZAAMBULIA PATUPU KWA KIPRE TCHETCHE ATAMBULISHWA OMAN

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Kipre Herman Tchetche ametambulishwa katika klabu ya Al-Nahda Al-Buraimi, Oman.
  Picha zimevuja mchezaji raia wa Ivoey Coast, Kipre Tchetche akiwa amevalia jezi za Al Nahda inayoshiriki Ligi Kuu ya Oman.
  Na Tchetche anaweka wazi kuhamia kwake Oman, baada ya mwishoni mwa wiki kuwa na mazungumzo na Mkurugenzi mmoja wa Azam FC, maana yake wamekubaliana aondoke.
  Lakini kusaini kwake Oman kunazima tetesi kwamba angekuja kuchezea klabu nyingine hapa Tanzania kati ya Simba na Yanga.
  Kipre Tchetche akikabidhiwa jezi ya Al nahda ya Oman baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Azam FC
  Mapema tu baada ya msimu kumalizika, Kipre Tchetche alisema kwamba hataki kuendelea kucheza Tanzania.
  Ukatokea mgogoro kidogo baina yake na Azam – klabu ikigoma kumuuza naye akisistiza kutaka kuondoka, kabla ya kufikia makubaliano na sasa wanaachana kwa salama.
  Kipre anaondoka Azam FC baada ya miaka mitano na anamuacha pacha wake na mdogo wake, kiungo Kipre Michael Balou waliyejiunga naye pamoja na timu hiyo mwaka 2011.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA ZAAMBULIA PATUPU KWA KIPRE TCHETCHE ATAMBULISHWA OMAN Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top