• HABARI MPYA

    Saturday, August 06, 2016

    SERENGETI BOYS YAWAKATAKLIA MADOGO WA SAUZI KWAO, SARE 1-1

    Na Alfred Lucas, JOHANNESBURG
    TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imelazimisha sare ya ugenini ya kufungana bao 1-1 na wenyeji Afrika Kusini Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Magharibi mwa Mji wa Johannesburg.
    Katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Tatu ya mchujo wa kuwania tiketi ya fainali za U-17 Madagascar mwakani, mabao yote yalipatikana kwa penalti kipindi cha pili.Afrika Kusini walianza kupata penalti katika dakika 65 iliyofungwa na Linamandlia Mchilizeli kabla ya Ally Msingi kuisawazishia Serengeti Boys katika dakika ya 70.
    Penalti ya Afrika Kusini ilitokana na mmoja wa mabeki wa Serengeti Boys kumfanyia madhambi Mchilizeli  wa Amajimbos ndani ya eneo la hatari wakati ile ya Serengeti Boys ilitoakana na beki Luke Donn wa Amajimbos kunawa mpira eneo la hatari.


    Kikosi cha Serengeti Boys kilicholazimisha sare na Amajimbos leo

    Afrika Kusini iliyoanza kwa kasi dakika 10 za mwanzo wa mchezo huo, ilipotea dakika zote 30 za kipindi cha kwanza ambao kukosa bahati na umakini kidogo tu kwa nyota wa Serengeti Boys kulisababisha kukosa mabao matano yakiwamo mawili yaliyogonga mwamba hivyo kuwatia hasira Serengeti Boys ambao walionyesha kuwa na njaa ya mabao.
    Kubanwa katika kipindi cha kwanza, kulisababisha Kocha Mkuu wa Amajimbos kufanya mabadiliko ya wachezaji wote watatu kipindi cha pili, wakati Bakari Shime kwa upande wake alimpumzisha Ibrahim na nafasi yake kuchukuliwa na Muhsin ambaye alisaidia kuendedlea kuwabana Afrika Kusini waliokjuwa wanawategemea nyota kama na Mswati Mavuso na Lethabo Mazibuko.
    Shukrani za pekee zinaweza kwenda kwa Kipa Ramadhani Kabwili aliyeokoa hatari nyingi ikiwamo mpira uliokuwa unakwenda golini uliotokana na adhabu ndogo. Kadhalika Msengi aliyekuwa nyota wa mchezo huo akimiliki vema idarta ya ulinzi akishirikiaana nDickson Job.
    Shime maarufu kama Mchawi Mweusi alisema: “Nashukuru kwa matokeo haya. Si mabaya kwangu. Tunarudi nyumbani kujipanga. Afrika Kusini ilikuwa inanitia hofu ndio maana nilisema mechi itakuwa ngumu.”
    Kwa upande wake, Naibu Balozi Rosemary alisema: “Ahsanteni vijana (Serengeti Boys) kwa kulinda heshima yangu,” wakati Malinzi alisema: “Sina mengi. Mkiwafunga Afrika Kusini Agosti 21, 2016 kambi inapigwa tena nje ya nchi. Sijui ni nchi gani, lakini mtakwenda kujiandaa nje ya nchi.”
    Kikosi cha Tanzania kilikuwa: Ramadhani Kabawili, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Ally Msengi, Dickson Job, Shaban Ada, Kelvin Naftal, Ally Ng’anzi, Ibrahim Abdallah/Muhsin Makame (Dakika ya 72), Asad Juma na Mohammed Rashid.
    Afrika Kusini: Glen Tumelo, Mswati Mavuso, Luke Donn, Sechaba Makoena, Kwenzokuhle Shinga, Mjabulise Mkhize, Bonga Dladla, Linamandla Mchilizeli, Luke Gareth, James Monyane na Siphamandla Ntuli.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAWAKATAKLIA MADOGO WA SAUZI KWAO, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top