BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limeendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kuinua sekta ya michezo nchini kwa kuhakikisha linawezesha timu za taifa na wana michezo mbalimbali kushiriki katika michezo ya taifa na ile ya kimataifa kwa ukamilifu huku likitoa fedha kiasi cha TZS. 5,829,403,959 katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo ya fedha ya 2023/2024 (TZS. 810,175,635), 2024/2025 (TZS. 3,803,566,185.) ambapo hadi kufikia Januari 2025/2026 tayari TZS. 1,215,662,139 zimekwisha tumika.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mtendaji wa BMT, Bi. Neema Msitha kuwa baadhi ya timu zilizowezeshwa ni Taifa ya Netiboli, Pooltable, Ngumi, Timu ya Mpira wa Miguu Taifa Stars iliyoshiriki mashindano ya CHAN yaliyofanyika katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda Agosti 2025, Timu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake “Twiga stars” iliyoshiriki mashindano ya WAFCON huko nchini Morroco Julai 2025 pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Watu Wenye Ulemavu “Amputee Football” walioshiriki mashindano ya Afrika Mashariki na Kati nchini Burundi Septemba, 2025.
Aeongeza kuwa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu Taifa Stars iliwezeshwa tena na kushiriki mashindano ya AFCON yaliyofanyika nchini Morocco Disemba 2025 na kufanikiwa kuingia 16 bora.
Amezitaja timu nyingine zilizowezeshwa kuwa ni pamoja na Singida Black Stars, Timu ya Taifa ya Kuogelea, Timu ya Mchezo wa Gofu wanawake, Timu ya Taifa ya paralimpiki, Timu ya taifa ya mpira wa wavu, Timu ya Judo na Timu ya Taifa ya Golfu.
Amesema timu ya riadha iliwezeshwa kushiriki mashindano ya Dunia Septemba, 2025 Jijini Tokyo, Japani ambapo Mwanariadha Alphonce Simbu alishinda na kupata medali ya Dhahabu pamoja na kushika nafasi ya pili katika mbio za Shanghai nchini China Novemba, 2023.
“Kwenye ngumi za Ridhaa, BMT iliwawezesha Bondia Grace Mwakamela na kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kutwaa medali ya fedha kwenye mashindano ya Afrika yaliyofanyika Yaounde nchini Cameroon mwaka 2023 huku Bondia Yusuf Changalawe akishinda medali ya Fedha katika mashindano Afrika ya kufuzu Olimpiki yaliyofanyika nchini Aprili 2024.



.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)


.png)
0 comments:
Post a Comment