• HABARI MPYA

    Tuesday, March 03, 2026

    FOUNTAIN GATE YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 PALE PALE SOKOINE

    TIMU ya Fountain Gate imepata ushindi wa ugenini wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Bao pekee la Fountain Gate lililoilaza Mbeya City nyumbani limefungwa na winga chipukizi wa umri wa miaka 19, Sadick Said Ramadhan dakika ya 79.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate inafikisha pointi 15 katika mchezo wa 15 na kupanda kwa nafasi mbili hadi ya 13, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 13 za mechi 15 pia nafasi ya 14 kwenye Ligi ya timu 16.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.  
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAICHAPA MBEYA CITY 1-0 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top