• HABARI MPYA

  Saturday, August 20, 2016

  NGASSA: NIKO FITI KAMA CHUMA, SASA NDIYO WASAUZI WATANIJUA

  Na Mwandisji Wetu, DAR ES SALAAM
  WAKATI Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini inatarajiwa kuanza wiki ijayo, kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa anayechezea Free State Stars amesema yuko fiti kama chuma.
  Ngassa aliyekuwa nje ya Uwanja kwa miezi miwili ya kuelekea mwisho wa msimu uliopita kutokana na kuwa majeruhi, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwamba anamshukuru Mungu kuelekea msimu mpya yuko vizuri kiasi cha kutosha.
  “Tumekuwa na kambi ya mwezi mmoja Johannesburg kujiandaa na msimu mpya na ninashukuru nimefanya mazoezi vizuri na wenzangu na ninajisikia vizuri kuelekea msimu mpya,”alisema.
  Mrisho Ngassa amesema yuko fiti kama chuma kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini

  Mfungaji huyo bora wa zamani wa Ligi ya Mabingwa Afrika amesema amedhamiria kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya ABSA kuanzia msimu huu baada ya kuwa na mwanzo wa kusuasua msimu uliopita.
  Free State watafungua dimba na wenyeji Chippa United Jumanne ya Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Nelson Mandela Bay kuanzia Saa 1:30 usiku.
  Ngassa alijiunga na Free State Stars msimu uliopita baada ya kumaliza Mkataba wake Yanga SC ya Tanzania. Hapa nchini, Ngassa mbali na Yanga amechezea klabu za Toto Africans, Kagera Sugar, Azam FC na Simba SC. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGASSA: NIKO FITI KAMA CHUMA, SASA NDIYO WASAUZI WATANIJUA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top