Lionel Messi alitangaza kustaafu soka ya kimataifa kwa sababu ya kufungwa fainali ya Copa America PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MWANASOKA bora wa dunia, Lionel Messi amebadilisha uamuzi wake wa kustaafu soka ya kimataifa na kurejea kuendelea kuichezea timu yake ya taifa, tena akisema anaipenda ile mbaya Argentina.
Nyota huyo wa Barcelona alitangaza kustaafu soka ya kimataifa mara tu baada kukosa penalti katika fainali ya Copa America dhidi ya Chile mwezi Juni, Argentina wakifungwa.
Pamoja na hayo, baada ya kukutana na kocha mpya wa timu ya taifa, Edgardo Bauza, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amethibitisha kurejea kikosini.
Messi, Nahodha wa Argentina na mfungaji bora wa kihistoria wa timu yake hiyo ya taifa kwa mabao yake 55, amesema katika taarifa yake amesema iliyochapishwa na gazeti la La Nacion: "Naona kuna matatizo mengi katika soka ya Argentina na sitaki kuongeza lingine moja. Sitaki kusababisha dosari yoyote,"alisema.
0 comments:
Post a Comment