• HABARI MPYA

  Wednesday, August 03, 2016

  MAVUGO ADUNDA UFARANSA, AAMUA KUREJEA SIMBA SC

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MPANGO wa mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, Ufaransa maarufu kama Ligue 2 umekwama na yuko njiani kuja Tanzania kujiunga na Simba SC.
  Mavugo alikwenda Ufaransa wakati tayari Simba SC wamesema wamekwishaingia Mkataba na mchezaji huyo kuanza kuwatumikia kuanzia msimu ujao.
  Habari ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE leo zinasema kwamba baada ya Mavugo kukwama Ufaransa, aliwasiliana na viongozi wa SImba SC na kukubaliana aje.
  Laudit Mavugo ametimkia Ufaransa wakati Simba wanamsubiri kambini Morogoro
  "Mavugo ameongea na Simba na wamemalizana, wamekubaliana aje na hivi ninavyokuambia anaweza kuwasili kuanzia leo,"kimesema chanzo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAVUGO ADUNDA UFARANSA, AAMUA KUREJEA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top