• HABARI MPYA

  Wednesday, August 03, 2016

  AZAM YAMTOA KWA MKOPO WINGA WA MEDEAMA

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  WINGA mpya wa Azam FC, Enock Atta Agyei aliyesajiliwa kutoka Medeama SC ya Ghana ataanza kuichezea timu hiyo Januari mwakani atakapotimiza umri wa miaka 18.
  Na japokuwa Azam FC imemnunua mchezaji huyo kutoka Medeama na kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, lakini inamrudisha Ghana kucheza kwa mkopo hadi Desemba.
  Habari za ndani ambazo BIN ZUBEIRY SPOIRTS – ONLINE imezipata zimesema kwamba Azam waliambiwa mapema juu ya mchezaji huyo na wakaridhia kumsaini waanze kumtumia Januari.

  Kocha Mkuu wa Azam FC, Mspaniola, Zeben Hernandez Rodriguez akimkabidhi jezi ya timu hiyo, winga Enock Atta Agyei kutoka Medeama SC ya Ghana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam juzi

  Lakini katika Mkataba waliosaini kuna kipengele cha mchezaji huyo kuuzwa iwapo atapata timu Ulaya wakati wowote, akiwa anacheza kwa mkopo Medeama au baada ya kujiunga na Azam FC.
  Kinda huyo aliwasili Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Jumapili akapokewa mazoezini na Kocha Mkuu Mspaniola, Zeben Hernandez Rodriguez Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM YAMTOA KWA MKOPO WINGA WA MEDEAMA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top