• HABARI MPYA

  Friday, August 12, 2016

  IGHALO AAMUA KUBAKI WATFORD HADI MWAKA 2021

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Nigeria, Odion Ighalo amekubali kusaini mpya wa miaka mitano na Watford.
  Ighalo ambaye amekuwa akitakiwa na West Brom, wanaosaka mshambuliaji mpya kabla ya kumruhusu Saido Berahino kuondoka, hivi karibu alitaka kuondoka katika klabu hiyo.
  Na The Baggies wakajaribu kumsajili mshambuliaji wa West Ham United Diafra Sakho, lakini akafeli vipimo vya afya, hivyo kulazimika kurejesha nguvu zao kwa Ighalo kumbembeleza abaki.
  Odion Ighalo amekubali kusaini mpya wa miaka mitano na Watford

  Mapema tu mwanzoni mwa dirisha hili la usajili, Watford ilikataa ofa ya Pauni Milioni 37.5 kutoka Shanghai SIPG ya China kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na sasa amejifunga na The Hornets.
  Mkataba wa awali Ighalo haukuwa wa kumalizika kabla ya mwaka 2020, lakini klabu hiyo imempa ofa nzuri mpya ili kumzuia kufikiria ofa za timu nyingine. Mkataba wake wa sasa utakwenda hadi mwaka 2021.
  Mnigeria huyo msimu uliopita alikuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Watford na amefunga mabao 15 katika Ligi Kuu ya England akicheza pamoja na Troy Deeney pale mbele, ambaye pia amesaini mkataba mpya wa miaka mitanio mwezi uliopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IGHALO AAMUA KUBAKI WATFORD HADI MWAKA 2021 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top