• HABARI MPYA

  Wednesday, August 03, 2016

  VICTORIA 92 ILISHEHENI WAKALI, LAKINI IKATUANGUSHA CHALLENGE MWANZA

  Wachezaji wa Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars wakiingia uwanjani kwa ajili ya mchezo wa Kombe la CECAFA Challenge dhidi ya Zambia Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza mwaka 1992. Stars ilifungwa 2-1 licha ya kutangulia kwa bao la Edibily Lunyamila dakika ya 11, Kelvin Mutale akasawazisha dakika ya 33 na kufunga la ushindi dakika ya 56. Stars iliokuwa Kundi B ilitolewa baada ya kushika nafasi ya tatu nyuma ya Malawi na Zambia, zilizofuzu Nusu Fainali. Timu nyingine katika kundi hilo, zilikuwa Zanzibar na Ethiopia. Timu B ya Tanzania, Kakakuona iliyokuwa Kundi A Arusha, ilifika hadi fainali na kufungwa na 1-0 na Uganda, bao pekee la Issa Sekatawa dakika ya 77.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VICTORIA 92 ILISHEHENI WAKALI, LAKINI IKATUANGUSHA CHALLENGE MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top