• HABARI MPYA

  Monday, May 16, 2016

  KENYA YAMUITA WA HISPANIA KUIVAA TAIFA STARS MEI 29 NAIROBI

  KOCHA wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Stanley Okumbi amemuita mzaliwa wa Hispania, Ismail Said Athuman Gonzalez anayechezea klabu ya CD Las Palmas ya La Liga na Bruce Kamau wa Melbourne City ya Ligi Kuu ya Australia.
  Wawili hao wataorodheshwa katika kikosi cha awali kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Tanzania mwishoni mwa mwezi huu.
  Gonzalez, mzaliwa wa Hispania kwa baba mama Mspanyola na baba Mkenya tayari amekubali mwaliko huo na anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Harambee Stars kambi itakapoanza.
  Kwa sasa, Mkenya huyo anacheza kwa mkopo klabu ya Cacereno ya Ligi Daraja la Kwanza, Segunda nchini Hispania.

  Ismail Said Athuman Gonzalez akiwa kazini na timu yake Las Palmas katika La Liga

  Kamau aliyezaliwa Kenya kabla ya kuhamia na wazazi wake Australia akiwa ana umri wa miaka minne, bado hajaamua achezee nchi ipi kutokana na zote Australia na Kenya kumuhitaji.
  “Nafikiri ni muhimu kuwaangalia wachezaji wote waliopo, wakiwemo hawa wawili,” amesema Okumbi.
  “Mazungumzo na Gonzalez yamekwenda vizuri sana, wakati Kamau bado hajafanya maamuzi kwa sababu na kule wanamtaka pi. Lakini tuna matumani ya kuwapata wote kwa ajili ya mchezo ujao wa kirafiki," amesema kocha huyo.

  Bruce Kamau wa Melbourne City ya Ligi Kuu ya Australia.

  Kenya inatarajiwa kucheza mechi mbili za kirafiki Uwanja wa Kasarani mjini Nairobi kujiandaa na mechi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Kongo nyumbani Juni 5.
  Kabla ya kucheza na Tanzania Mei 29, Harambee Stars itacheza na Sudan.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KENYA YAMUITA WA HISPANIA KUIVAA TAIFA STARS MEI 29 NAIROBI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top