• HABARI MPYA

    Sunday, May 22, 2016

    NIYONZIMA, MUGIRANEZA WAITWA RWANDA KUZIVAA SENEGAL, MSUMBIJI

    KOCHA wa Rwanda, Johnathan McKinstry ameteua wachezaji 29 katika kikosi chake cha awali kwa ajili ya mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika Kundi H dhidi ya Msumbiji Jumamosi ya Juni 4, in Kigali.
    Sura mpya katika kikosi hicho ni pamoja nyota wawili wa Rayon Sports, Emmanuel Imanishimwe na Thiery Manzi, kiungo Ali Niyonzima wa Mukura VS na Patrick Sibomana wa APR.
    Wachezaji wanne wanaocheza nje wamejumuishwa pia wakiwemo viungo, Nahodha Haruna Niyonzima wa Yanga, Jean Baptista Mugiraneza wa Azam FC za Tanzania, beki wa kushoto Abouba Sibomana na mshambuliaji Jacques Tuyisenge wote wa Gor Mahia ya Kenya, Salomon Nirisarike Sint-Truiden ya Ubelgiji na Elias Uzamukunda wa Le Mans ya Ufaransa.
    Haruna Niyonzima (kulia) akimtoka Jean Baptiste Mugiraneza katika mchezo kati ya Yanga na Azam FC msimu uliopita

    Wachezaji maarufu waliotemwa ni Quentin Rushenguziminega anayechezea Lausanne Sport ya Uswisi.
    Katika kujiandaa na mchezo dhidi ya Msumbiji, Amavubi itamenyana Senegal katika mchezo wa kirafiki Jumamosi ya Mei 28 mjini Kigali na Mckinstry atatumia mchezo huo kupata kikosi cha mwisho.
    Rwanda kwa sasa inashika nafasi ya pili katika Kundi H ikiwa na pointi sita, sawa na Ghana, ambao watamenyana nayo katika mchezo wa mwisho wa kuamua timu ya kufuzu AFCON  Septemba.
    Kikosi kamili cha Amavubi kinaundwa na makipa; Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Andre Mazimpaka (Mukura), Jean Claude Ndoli (APR), Marcel Nzarora (Polisi)
    Mabeki; Michel Rusheshangoga (APR), Fitina Omborenga (SC Kiyovu), Celestin Ndayishimiye (Mukura), Abouba Sibomana (Gor Mahia, Kenya), Emmanuel Imanishimwe (Rayon Sports), Nirisrike Salomon (Sint-Truiden, Ubelgiji), Emery Bayisenge (APR), Abdul Rwatubyaye (APR), Kayumba Soter (AS Kigali), Manzi Thierry (Rayon Sports)
    Viungo; Djihad Bizimana (APR), Imran Nshimiyimana (Polisi), Jean Baptiste Mugiraneza (Azam FC, Tanzania), Yannick Mukunzi (APR), Ali Niyonzima (Mukura), Innocent Habyarimana (Police), Patrick Sibomana (APR), Jean Claude Iranzi (APR), Hakizimana Muhadjiri (Mukura), Dominique Savio Nshuti (Rayon Sports), Habimana Yussufu (Mukura), Haruna Niyonzima (Yanga SC, Tanzania)
    Washambuliaji; Danny Usengimana (Polisi), Elias Uzumakunda (Le Mans, Ufaransa), Jacques Tuyisenge (Gor Mahia, Kenya), Ernest Sugira (AS Kigali).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIYONZIMA, MUGIRANEZA WAITWA RWANDA KUZIVAA SENEGAL, MSUMBIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top