• HABARI MPYA

    Tuesday, May 31, 2016

    'MCHEZAJI MPYA' WA MAN UNITED ATEMWA KIKOSI CHA HISPANIA EURO 2016

    KIUNGO wa Atletico Madrid, Saul Niguez, anayetakiwa kwa dau la Pauni Milioni 54 na kocha Jose Mourinho wa Manchester United, hajajumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha Hispania cha Euro 2016.
    Kinda huyo wa umri wa miaka 21, aliyecheza vizuri fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakifungwa na Real Madrid kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 1-1, ametemwa kwenye kikosi cha mwisho cha Hispania pamoja na Isco.
    Baada ya awali kuteua kikosi cha wachezaji 19, kocha Vicente del Bosque ametaja wachezaji wanne wa kukamilisha orodha ya wachezaji 23 akiwachukua Sergio Ramos, Juanfran, Lucas Vazquez na Koke - ambaye pia alicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa San Siro Jumamosi.
    Kiungo anayetakiwa Manchester United, Saul Niguez hajachukuliwa kikosi cha Hispania cha Euro 2016  PICHA ZAIDI GONGA HAPA   

    KIKOSI CHA MWISHO CHA HISPANIA EURO 2016

    Makipa: Iker Casillas (Porto), David De Gea (Man United), Sergio Rico (Sevilla)
    Mabeki: Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique, Jordi Alba, Marc Bartra (all Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Mikel San Jose (Athletic Bilbao), Hector Bellerin (Arsenal), Juanfran (Atletico Madrid)
    Viungo: Bruno (Villarreal), Sergio Busquets, Andres Iniesta (both Barcelona), Thiago (Bayern Munich), David Silva (Manchester City), Pedro, Cesc Fabregas (both Chelsea), Lucas Vazquez (Real Madrid), Koke (Atletico Madrid)
    Washambuliaji: Aritz Aduriz (Athletic Bilbao), Nolito (Celta Vigo), Alvaro Morata (Juventus)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: 'MCHEZAJI MPYA' WA MAN UNITED ATEMWA KIKOSI CHA HISPANIA EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top