• HABARI MPYA

    Friday, May 27, 2016

    AZAM TV YAMWAGA BILIONI 2 TFF KWA AJILI YA LIGI KUU YA VIJANA U-20 NA WANAWAKE

    Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
    KAMPUNI ya Azam Media Limited leo imeingia Mkataba na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) wenye thamani ya Sh. Bilioni 2 kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania na Ligi Kuu ya Vijana wa umri chini ya miaka 20.
    Zoezi hilo limefanyika Ofisi za makao Makuu ya Azam Media Ltd eneo la TAZARA, Dar es Salaam upande wa TFF ukiwakilishwa na Rais wake, Jamal Malinzi na Azam Media wakiwakilishwa na Mtendaji wake Mkuu, Muingereza Rhys Torrington.
    Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Torrington amesema Mkataba huo ni wa miaka mitano na lengo laoe ni kuendelea kusaidia kuinua michezo Tanzania.
    Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington (wa pili kulia) akibadilishana mikataba na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (wa pili kushoto) baada ya kusiani leo. Wengine kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Soka ya Wanawake, Rose Kisiwa na Rais wa Kamati hiyo, Amina Karuma
    Malinzi na Torrington wakisaini mikataa hiyo, huku wakishuhudiwa na Rais wa Chama cha Soka ya Wanawake (TWFA), Amina Karuma 
    Rais wa TWFA, Amina Karuma akiwashukuru Azam Media kwa hisia leo TAZARA

    "Baada ya mafanikio ya awali tukiwa na Ligi Kuu ya Wanaume na mashindano mengine, sasa tunapiga hatua nyingine hatika jitihada zetu kuchangia maendeleo ya soka nchini kwa kuingia mikataba ya ligi hizi mbili,"amesema Torrington.
    Kwa upande wake, Malinzi amesema kwamba Ligi Kuu ya Wanawake itaanza kwa kushirikisha klabu 10 Agosti mwaka huu na Ligi ya U20 itashirikisha klabu zote za Ligi Kuu ya Wanaume.
    "Na Ligi ya U20 itachezwa sambamba na Ligi Kuu ya wanaume, kabla ya mechi za timu za wakubwa, zitatangulia mechi za vijana. Na kila timu itasafirisha timu yake ya vijana kwa mechi za mikoani. Itakuwa ligi kamili na yenye kanuni madhubuti,"amesema Malinzi. 
    Malinzi amesema Ligi ya Wanawake itaanza na timu 10 baada ya hapo Chama Cha Soka ya Wanawake (TWFA) kitatengeneza muundo wa timu kupanda na kushuka.
    Kuhusu Ligi ya vijana, Malinzi amesema wataunda kanuni kali za Ligi Kuu kuhakikisha klabu zote za ligi hiyo zinashiriki kikamilifu na kwamba klabu itakayoshindwa kuingiza kikosi cha vijana uwanjani itakatwa pointi tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara  
    Malinzi amesema kila klabu ya Ligi Kuu itawajibika kuwa na timu ya U20 kama ilivyo Ada kanuni za uendeshaji wa mashindano haya zitatungwa na TFF na Ligi hizi zitaanza msimu wa 2016/2017.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TWFA, Amina Kaluma ameishukuru Azam Media Limited kwa kudhamini Ligi Kuu ya Wanawake na kumpongeza Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa jitihada za kufanikisha dili.
    Azam Media Ltd imekuwa ikishirikiana na TFF katika kukuza na kuboresha Tasnia ya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kwa kuingia mikataba kama hii ya urushaji wa matangazo ya moja kwa moja katika Ligi Kuu Taznania Bara na Kombe la Shirikisho, maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC).
    Licha ya hivyo Azam Media Ltd imekuwa ikidhamini pamoja na kununua haki za kurusha matangazo ya ligi za mpira wa miguu nje ya nchi kama Uganda (AUPL), Rwanda (ARFC) na Kenya, ikiwa na dhumuni la kuendeleza na kuboresha kiwango cha soka katika ukanda wa Afrika Mashariki.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM TV YAMWAGA BILIONI 2 TFF KWA AJILI YA LIGI KUU YA VIJANA U-20 NA WANAWAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top