• HABARI MPYA

    Tuesday, May 31, 2016

    MUDA WA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA YANGA WAONGEZWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans, maarufu Yanga imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
    Katika kikao chake cha kufanya tathmini kilichoketi jioni ya leo Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu hadi Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.
    Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kulia atalazimika kutetea nafasi yake katika uchaguzi

    Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
    Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
    Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
    Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni tarehe 6 Juni, 2016. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MUDA WA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA YANGA WAONGEZWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top