• HABARI MPYA

    Monday, May 30, 2016

    MKWASA: MISRI WANAFUATA SARE, LAKINI TUTAWAPIGA

    Na Alfred Lucas, NAIROBI
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.
    Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo kati ya Harambee Stars ya Kenya na Taifa Stars ya Tanzania Mei 29, 2016, uliofanyika Uwanja wa Moi Kasarani, Mkwasa maarufu kama Master anasema kwa msimamo na hali ilivyo kwa sasa, “Najua Misri wanatufuatilia. Na hata Kenya kwa siku zote tatu walikuwako. Najua  Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizi, lakini hawataipata Tanzania.”
    Mkwasa amesema Misri wanafuata sare Dar es Salaam ili kujihakikishia tiketi ya AFCON
    Mkwasa anasema mchezo dhidi ya Misri, ana uhakika vijana wake watajitahidi ili kupata matokeo mazuri baada ya Jumapili kufanya vema dhidi ya Harambee Stars waliocheza mechi hiyo mbele ya mashabiki wao wachache ambao pia hawakuchangamka kama wale wa Tanzania ambao licha ya kuwa ugenini walichangamsha mji na uwanja.
    Wakati Misri wana pointi saba, Taifa Stars ina pointi moja na hivyo wa kuibania au kupindua matokeo ya Misri isiende AFCON mwakani, basi ni Tanzania hasa kama itawafunga Mapharao Jumamosi kabla ya kwenda Nigeria Septemba, mwaka huu kucheza na Nigeria.
    “Kama nilivyosema, Misri wanakujawanahitaji pointi moja. Lakini sisi tunahitaji pointi tatu. Mchezo wa leo unatosha kuona mapungufu (upungufu). Maana ilikuwa mechi ngumu iliuyojaa nyota wote wa Kenya ambao ni professionals, lakini mimi nilikuwa na local based players na matokeo yamekuwa hayo.
    “Tilianza kufunga bao, lakini wakarudisha. Bora mchezo umeishia hivi maana najua Wakenya hawana uvumilivu, tungewafunga hapa sijui kama tungetoka salama,” amesema Mkwasa ambaye baadhi ya waandishi, hususani wale wa Kenya walianguka kicheko kuashiria kuwa kuna matatizo katika utawala wa soka.
    Mkwasa anasema ana taarifa namna ambavyo Misri wanaifuatilia Taifa Star hususani ukusanyaji wa video kwa ajili ya kuona aina ya soka la Tanzania, huku akisema: “Hawatafanikiwa kwa sababu soccer is the game of different approach (Soka ni mchezo wenye mifumo tofauti). Hivyo tulivyocheza na Kenya sivyo nitakavyocheza na Misri, nitakuwa na approach yake.”
    Anasema ushindi wa Jumamosi ijayo ni wa kuvuna pointi tatu ili kupata kasi ya kushinda mchezo dhidi ya Nigeria na kufungua ukurasa mpya wa Taifa Stars kutengeneza mazingira mazuri ya kuwashinda Nigeria katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi utakaofanyika Septemba, mwaka huu.
    “Tunaomba Wakenya mtuombee. Nasi tunawaombea ili kama wote inatokea mwaka huu tunakosa mafasi, basi iwe kheri kwa kipindi kijacho. Sisi tumekuja kucheza kwenu katika mji wenu wenye baridi basi nanyi karibuni siku moja dar es Salaam, Tanzania katika mji wetu wetu wenye joto, huenda mkaambulia sare vile vile,” anasema.
    Mkwasa alipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (FKF), kwa kuandaa mchezo huo angalau kwa asilimia 70 kwa kushirikiana na Tanzania iliyojazia gharama za juu sambamba vijana wake kwa kucheza kwa kujituma licha ya kuwakosa nyota wake wa kulipwa na hivyo kupata picha na mbinu sahihi za kuivaa Misri Jumamosi ijayo.
    “Bado tunaendele kujenga timu yetu, wengi ni vijana kama mlivyoona na wengine ni mara ya kwanza wanacheza. Nimewapa nafasi na mmeona uwezo wao, bila shaka tutafanya vema maana wengine ni under 21 wako kwenye kikosi. Huko mbele tutakuwa na timu nzuri,” anasema Mkwasa akimtolea mfano Shiza Ramadhani ambaye alipewa nafasi kwa mara ya kanza katika kikosi cha kwanza akichukua winga ya kulia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA: MISRI WANAFUATA SARE, LAKINI TUTAWAPIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top