• HABARI MPYA

    Wednesday, May 25, 2016

    TIMBWILI LA MAANA AZAM NA YANGA TAIFA LEO

    MECHI ZILIZOPITA ZA AZAM NA YANGA:
    Machi 5, 2016 
    Yanga 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Taifa)
    Januari 5, 2016 
    Yanga SC 1-1 Azam (Kombe la Mapinduzi)
    Oktoba 17, 2015 
    Yanga SC 1-1 Azam (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Agosti 22, 2015
    Yanga 0-0 Azam FC (Yanga ilishinda kwa penalti 8-7 Ngao ya Jamii)
    Julai 29, 2015
    Azam 0-0 Yanga SC (Azam ilishinda kwa penalti 5-3 Robo Fainali Kombe la Kagame)
    Mei 6, 2015
    Azam 2-1 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Desemba 28, 2014
    Yanga SC 2-2 Azam (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Septemba 14, 2014
    Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
    Machi 19, 2014; 
    Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Septemba 22, 2013; 
    Azam FC 3-2 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Februari 23, 2013;  
    Yanga SC 1-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
    Novemba 4, 2012;  
    Azam FC 0-2 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Machi 10, 2012; 
    Yanga SC 1-3 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    January 07, 2012
    Azam FC 3-0 Yanga SC (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
    Septemba 18, 2011;  
    Azam 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Machi 30, 2011;  
    Yanga SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Oktoba 24, 2010; 
    Azam FC 0-0 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Machi 7, 2010;  
    Yanga SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Oktoba 17, 2009; 
    Azam FC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Aprili 8, 2009;  
    Yanga SC 2-3 Azam FC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    Oktoba 15, 2008;  
    Azam FC 1-3 Yanga SC (Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara)
    (Rekodi hii inahusisha mechi za mashindano tu, tangu Azam na Yanga wanaanza kukutana)

    Winga wa Azam FC, Farid Mussa (kulia) akiwafunga tela mabeki wa Yanga SC, Juma Abdul (katikati) na Nadir Haroub 'Cannavaro' (kushoto) katika moja ya mechi zilizopitaa baina ya timu hizo msimu huu

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAPINZANI wakuu wa mataji nchini, Azam FC na Yanga wanakutana jioni ya leo katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Yanga inashuka uwanjani leo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuizidi kete Azam FC katika mataji mawili, kwanza Ngao ya Jamii Agosti 22, mwaka jana waliposhinda kwa penalti 8-7 baada ya sare ya 0-0 na baadaye katika Ligi Kuu, ingawa timu hizo zilitoa sare mechi zote mbili, kwanza 1-1 Oktoba 17, mwaka jana na baadaye 2-2 Machi 5, mwaka huu.
    Mchezo mwingine uliozikutanisha Yanga na Azam msimu huu ni wa Kombe la Mapinduzi ambao pia zilitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
    Ndani ya dakika 90, hakuna mechi ya Yanga na Azam FC imetoa mbabe msimu huu na mchezo wa leo kwa kuwa ni wa fainali, unaweza kufika kwenye mikwaju ya penalti pia.
    Kwa mara ya kwanza msimu huu, Azam itakutana na Yanga katika bechi la Ufundi kukiwa na mabadiliko, baada ya kundolewa Muingereza Stewart John Hall na timu yake na kuajiriwa Mspanyola Zebensul Hernandez Rodriguez na timu yake.
    Yanga itaendelea kuwa chini ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ambaye alitaka kugombana na kocha wa Azam katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu Zanzibar.
    Mchezo huo utachezeshwa na refa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam, ambaye atasaidiwa na Ferdinand Chancha wa Mwanza na Soud Lila wa Dar es Salaam wakaopeperusha vibendera, wakati mezani atakuwapo Frank Komba wa Dar es Salaam pia na Kamisaa ni mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Juma Mgunda wa Tanga.
    Tayari TFF imekwishaitangaza Azam FC  itacheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, kwa kuwa Yanga tayari wana tiketi ya Ligi ya Mabingwa, hivyo fainali ya leo ya Kombe la ASFC itatuhitimishia msimu na kupata fursa ya kujua mbabe baina ya timu hizo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMBWILI LA MAANA AZAM NA YANGA TAIFA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top