• HABARI MPYA

    Friday, May 27, 2016

    HUYU HAPA MOURINHO NA UZI WA MAN UNITED, ZAMA MPYA OLD TRAFFORD

    KLABU ya Manchester United imemtangaza rasmi Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya, akirithi mikoba ya Mholanzi, Louis Van Gaal aliyeondolewa wiki iliyopita.
    Kocha huyo amesaini Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 45 na atapewa Pauni Milioni 200 kwa ajili ya ajili ya usajili kuelekea msimu mpya.
    Na Mreno huyo ametua Man United kutokana na klabu hiyo kuvutiwa na wasifu wake mzuri akiwa ameshinda mataji yote ya Ulaya na Ligi za Serie A ya Italia, Ligi Kuu ya England na La Liga ya Hispania.
    Benfica ndiyo ilikuwa timu yake ya kwanza, ambako baada ya mechi 11, aliweka rekodi ya ushindi wa asilimia 54.55 kabla ya kuhamia Uniao de Leiria.

    Kocha Jose Mourinho akiwa na jezi ya Man United baada ya kutambulishwa rasmi kuwa kocha timu hiyo leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA


    Na baada ya mechi 20, akachukuliwa na Porto na huko ndiko rasmi umaarufu wake kama kocha ulipoibukia.
    Ilimchukua Mourinho misimu miwili tu kufanya ambacho hakikufikiriwa baada ya kuwaongoza vigogo hao wa Ureno kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiifunga Monaco ya Ufaransa kwenye fainali. 
    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 baada ya mafanikio hayo akajipa 'Special One' wakati anawasili Chelsea na akapata umaarufu zaidi baada ya kushinda mataji katika misimu yake miwili ya mwanzo Stamford Bridge.
    Pia ameshinda mataji ya Kombe la FA na mawili ya Kombe la Ligi England, lakini mmiliki wa Chelsea, bilionea Mrusi Roman Abramovich akamuondoa kazini. 
    Mreno huyo akahamia Serie A ambako akashinda taji katika msimu wake wa kwanza kabla ya kuiongoza Inter Milan kutwaa mataji msimu uliofuata, likiwemo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
    Mourinho akaenda kuwa kocha wa 11 wa Real Madrid ndani ya miaka saba na kufanikiwa kuzima ubabe wa Barcelona kutwaa mfululizo mataji ya La Liga kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Hispania, katika msimu wake wa pili. 
    Hakuweza kutwaa taji la Ulaya na akashindwa kutwaa taji lolote katika msimu wake wa mwisho na akaondoka kwa makubaliano mazuri, kabla ya kurejea Chelsea ambako katika msimu wake wa kwanza akashika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu kabla ya kushinda taji hilo katika msimu uliofuata na kusaini Mkataba mpya hadi mwaka 2019.
    Lakini mwanzo wa msimu wa 2015-16 haukuwa mzuri kwa Mourinho baada ya kuandamwa na matokeo mabaya hadi akaondolewa

    MATAJI ALIYOSHINDA MOURINHO
    Porto (Mataji 6)
    Januari 2002 - Mie 2004
    Primeira Liga: 2002-03, 2003-04
    Taca de Portugal: 2002-03
    Supertaca Candido de Oliveira: 2003
    UEFA Champions League: 2003-04
    UEFA Cup: 2002-03

    Chelsea  (Mataji6)
    Juni 2004 - Septemba 2007 
    Premier League: 2004-05, 2005-06
    FA Cup: 2006-07
    League Cup: 2004-05, 2006-07
    FA Community Shield: 2005

    Inter Milan (Mataji 5)
    Juni 2008 - Mei 2010 
    Serie A: 2008-09, 2009-10
    Coppa Italia: 2009-10
    Supercoppa Italiana: 2008
    UEFA Champions League: 2009-10

    Real Madrid (Mataji 3)
    Mei 2010 - June 2013
    La Liga: 2011–12
    Copa del Rey: 2010–11
    Supercopa de Espana: 2012

    Chelsea (Mataji 2)
    June 2013 - December 2015 
    Premier League: 2014-15
    League Cup: 2014-15

    Tuzo na mataji binafasi
    Kocha Bora wa Mwaka wa Onze d'Or: 2005
    Kocha Bora wa Dunai wa FIFA: 2010
    Kocha Bora wa IFFHS: 2004, 2005, 2010, 2012
    Kocha Bora wa Ligi Kuu England wa Mwaka; 2004–05, 2005–06, 2014–15 
    Kocha Bora wa Mwaka wa Serie A: 2008–09, 2009–10 
    Kocha Bora wa Mwaka wa UEFA: 2002–03, 2003–04
    Timu Bora ya Mwaka ya UEFA: 2003, 2004, 2005, 2010 
    Kocha Bora wa BBC Sports Personality wa Mwaka; 2005
    Mwanamichezo Bpra wa La Gazzetta dello Sport: 2010 Kocha Bora wa Karne wa Ureno: 2015 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HUYU HAPA MOURINHO NA UZI WA MAN UNITED, ZAMA MPYA OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top