• HABARI MPYA

  Thursday, March 17, 2016

  VODACOM YAMJAZA MANOTI KAMUSOKO

  KAMPUNI ya Vodacom Tanzania, wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara leo wamemkabidhi kitita cha Tsh Milioni 1 kiungo wa Yanga, Thaban Kamusoko baada ya kuibuka Mchezaji bora wa ligihiyo kwa mwezi Desemba 2015. 
  Mzimbabwe huyo mwenye rasta kichwani, aliibuka mshindi baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Amiss Tambwe, raia wa Burundi.
  Kamusoko aliisadia timu yake ya Yanga kupata ushindi katika michezo iliyochezwa mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika mechi tatu zilizochezwa mwezi huo.
  Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Milioni 1 kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko (wa pili kushoto) baada ya kuibuka Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Desemba mwaka jana. Wengine kulia ni Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh na Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi

  Zawadi ya kitita alikabidhiwa na Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya wakati timu hiyo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kujiandaa na mechi yao ya Jumamosi dhidi ya APR ya Rwanda Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Katika mahojiano aliyofanya na Vodacom Tanzania, Kamusoko ameishukuru kampuni hiyo kwa kudhamini ligi kuu Vodacom Tanzania na kuwezesha kuonesha kipaji chake pia kwa kumkabidhi zawadi ya fedha taslimu Tsh Milioni 1. Kamusoko amewashukuru pia mashabiki wa timu yake kwa kuendelea kuwasapoti wachezaji na amesema anawapenda na anawaamini sana. 
  Kamusoko amekuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga

  "Ninaimani kila timu inapocheza na Yanga inatamani kutufunga, hivyo ninawaomba mashabiki wawe wavumilivu, lakini tunawahakikishia ushindi kila tunapocheza kwenye uwanja huu” amesema Kamusoko.
  Naye kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi alisema; "Kwanza niipongeze timu yote kwa ujumla, na ninaipongeza wahusika kwa sababu wamemchagua mchezaji ambaye ana vigezo vyote vya kuweza kuwa mchezaji wa Yanga,”. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: VODACOM YAMJAZA MANOTI KAMUSOKO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top