• HABARI MPYA

    Tuesday, March 29, 2016

    TFF YAZIKAZIA AZAM NA YANGA ZICHEZE KOMBE LA SHIRIKISHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOMBE la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) linatarajiwa kuendelea Alhamisi kwa michezo miwili kuchezwa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
    Azam FC watakua kwenye uwanja wa Azam Complex kuwakaribisha maafande wa Tanzania Prisons siku ya Alhamis saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
    Yanga SC watakua wenyeji wa Ndanda FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kila timu ikihitaji ushindi katika michezo hiyo ili kuweza kufuzu kwa hatua ya nusu fainali.
    Aprili 11, Simba SC watakamilisha hatua ya robo kwa fainali kwa kucheza na wagosi wa kaya Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Benchi la Ufundi la Azam FC litakuwa na mchezo wa Kombe la TFF Alhamisi

    Mwadui FC ndio timu pekee mpaka sasa ambayo imeshafuzu kwa hatua ya nusu fainali, baada ya kuwachapa Geita Gold kwa mabao 3 -0.
    Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) atawakilisha Tanzania mwakani kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAZIKAZIA AZAM NA YANGA ZICHEZE KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top