• HABARI MPYA

    Wednesday, March 23, 2016

    RATIBA LIGI KUU KUFUMULIWA TENA

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kwamba watalazimika kupangua Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iwapo Azam na Yanga zitasonga mbele kwenye michuano ya Afrika.
    Azam watamenyana na Esperance ya Tunsia katika Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho na wakifanikiwa kuitoa timu hiyo, watakwenda kwenye mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.
    Yanga watamenyana na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na wakiitoa watakwenda hatua ya makundi wakati wakitolewa watahamia kwenye mchujo wa kuwania tiketi ya makundi ya kombe la Shirikisho.

    Na kwa sababu hiyo, Wambura amesema; 
    “Iwapo Azam itasonga mbele itacheza mechi hizo za mtoano, wakati Yanga yenyewe itacheza tu mechi hizo za mtoano iwapo itatolewa katika raundi inayofuata ya Ligi ya Mabingwa,”. 
    “Hivi sasa Azam na Yanga zinashiriki hatua ya 16 bora ambayo itachezwa kati ya Aprili 8-10 kwa mechi za nyumbani, na Aprili 19 na 20 kwa mechi za ugenini,”.
    “Mechi za kwanza za raundi ya mtoano (play offs) zitachezwa kati ya Mei 6-8 wakati za marudiano zitafanyika Mei 17-18. Yanga ikiitoa Al Ahly maana yake haitacheza hatua ya mtoano (play offs), na badala yake itasubiri moja kwa moja hatua ya makundi ambayo mechi zake za kwanza zitafanyika kati ya Juni 17-19,”.
    “Marekebisho mengine yanaweza kufanyika kwa kuzingatia matokeo ya scenario hizo hapo juu,”.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RATIBA LIGI KUU KUFUMULIWA TENA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top