• HABARI MPYA

    Sunday, March 27, 2016

    KIPA WA SIMBA, ABBEL DHAIRA AFARIKI DUNIA

    Dhaira siku za mwisho za uhai wake
    KIPA wa zamani wa Simba SC, Abbel Dhaira amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na ugojwa wa saratani ya tumbo kwa muda mrefu.
    Kipa huyo wa kimataifa wa Uganda, amefariki akiwa nna umri wa miaka 28 nchini Iceland, ambako alikuwa anachezea klabu ya IBV Vestmannaeyjar.
    Mlinda mlango huyo aliyezaliwa Septemba 9, mwaka 1987, Dhaira amechezea klabu za AS Vita ya DRC, Express na URA za kwao, Uganda, Simba ya Tanzania na IBV ya Iceland.
    Abbel Dhaira (kulia) akibadilishana mikataba na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe wakati anasajiliwa Msimbazi mwaka 2013
    Dhaira amekuwa akilazwa na kuruhusiwa hospitali kwa muda kutokana na saratani ya tumbo ambayo imekatisha maisha yake ya soka.
    Dhaira aliyechezea Simba kwa msimu mmoja wa 2013/2014 kabla ya kurejea Ulaya, alianza kupatiwa matibabu mapema mwaka huu baada ya klabu yake, IBV Vestmannaeyjar kuchangisha fedha kwa ajili hiyo, lakini wakati huo hali yake tayari ilikuwa mbaya sana.
    Dhaira, alianza kuchezea timu ya taifa ya Uganda mwaka 2009 na akacheza Kombe la CECAFA Challenge mwaka 2012, ambako alikimbizwa hospitali na kulazwa baada ya kuzimia kufuatia kugongana na mchezaji mwenzake. Pole kwa familia yake na Waganda wote. Mungu ampumzishe kwa amani Dhaira. Mbele yake, nyuma yetu. Amin.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIPA WA SIMBA, ABBEL DHAIRA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top