• HABARI MPYA

    Thursday, March 31, 2016

    KAPOMBE APANIA MAKUBWA BAADA YA TUZO YA VODA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BEKI wa Azam FC ya Dar es Salaam, Shomary Kapombe jana amekabidhiwa kitita cha shilingi Milioni 1/- kutokana na kuibuka mchezaji bora wa Ligi ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Januari mwaka huu.
    Kapombe alikabidhiwa kitita hicho  kutoka kwa mdhamini wa wa ligi hiyo, Vodacom Tanzania jana Uwanja  wa Azam Complex, Chamanzi, Dar es Salaam.
    Akizungumza baada ya kukabidhiwa  zawadi hiyo  ikiwa ni tuzo ya uchezaji bora,Kapombe alisema amefurahia kuwa miongoni mwa wachezaji waliopata tuzo tuzo na kuongeza kuwa imezidi kumtia moyo na bidii ya kujituma zaidi.
    “Nashukuru Vodacom kwa kuwapatia zawadi wachezaji wanaofanya vizuri kwa kuwa inawazidishia kasi ya kujituma zaidi, pia nawashukuru wachezaji wenzangu wote wa Azam maana bila  jitihada za pamoja sio rahisi mchezaji mmoja ukaibuka na kuonekana bora kwa kuwa katika mchezo wa soka sote tunategemeana” alisema.
    Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu aliyeambatana na Ofisa wa Bodi ya Ligi, Joel Balisidya pamoja na Ofisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo, Ibrahim Kaude katika kumkabidhi zawadi hiyo alimpongeza mchezaji huyo na kuongeza kusema kuwa Vodacom inajivunia mafanikio yanayoendelea kupatikana katika ligi hiyo na ina mpango wa kushirikiana na wadau wengine wa soka kuzidi kuiboresha zaidi.
    Shomary Kapombe amepania kuendelea kufanya vizuri Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara

    VIDEO; KAPOMBE AKIIZUNGUMZIA TUZO YAKE


    Kapombe alitwaa tuzo  mwezi Januari uliokuwa na raundi tatu, alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting.
    Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari 24, 2016.
    Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, na mara nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake.
    Washindani wa Kapombe kwenye kinyang'anyiro hicho katika mwezi huo walikuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAPOMBE APANIA MAKUBWA BAADA YA TUZO YA VODA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top