• HABARI MPYA

    Thursday, March 24, 2016

    RAFIKI WA BIN ZUBEIRY, JOHAN CRUYFF AFARIKI DUNIA

    Johan Cruyff (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, Mahmoud Zubeiry enzi za uhai wake alipozuru Tanzania mwaka jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    HISTORIA YA JOHAN CRUYFF 

    MCHEZAJI 
    Ajax (1964-73) – Mechi 240 mabao 190 
    Barcelona (1973-78) – Mechi 143 mabao 48 
    LA Aztecs (1979-80) – Mechi 23 mabao 13 
    Washington Diplomats (1980-81) – Mechi 30 mabao 12
    Levante (1981) – Mechi 10 Mabao 2 
    Ajax (1981-83) – Mechi 36 Mabao 14 
    Feyenoord (1983-84) – Mechi 33 Mabao 11 
    Uholanzi (1966-77) – Mechi 48 Mabao 33 
    KOCHA
    Ajax (1985-88)
    Barcelona (1988-96)
    Catalonia (2009-13)
    GWIJI wa soka, Mholanzi Johan Cruyff amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 68.
    Cruyff, ambaye aliichezea mechi 48 Uholanzi pamoja na klabu za Ajax ya kwao na Barcelona ya Hispania, amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani.
    Taarifa katika tovuti yake imesema; "Machi 24 mwaka 2016 Johan Cruyff (miaka 68) amefariki dunia kwa amani mjini Barcelona, akiwa amezungukwa na famili yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani,".
    "Ilikuwa ni huzuni kubwa na tunakuomba uheshimu siri za familia katika wakati huu mgumu,".
    Cruyff,ambaye ameshinda mataji matatu ya Ulaya na manane ya Uholanzi akiwa na Ajax, ameanza kusumbuliwa na saratani tangu Oktoba mwaka jana.
    Aprili mwaka jana, Cruyff alizuru Tanzania pamoja na kikosi cha Maveterani wa Barcelona ambao walicheza mechi ya wachezaji wa zamani nchini Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAFIKI WA BIN ZUBEIRY, JOHAN CRUYFF AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top