• HABARI MPYA

  Friday, March 18, 2016

  LIVERPOOL YAITUPA NJE MAN UNITED ULAYA

  MATOKEO MECHI ZA UEFA EUROPA LEAGUE
  Machi 17, 2016  
  Sevilla 3-0 FC Basel (3-0)
  RSC Anderlecht 0-1 Shakhtar Donetsk (1-4)
  Manchester United 1-1 Liverpool (1-3)
  Tottenham Hotspur 1-2 Borussia Dortmund (1-5)
  Valencia CF 2-1 Athletic Club (2-2, Athletic imefuzu kwa bao la ugenini, Sparta Prague (1-4
  Lazio 0-3 Sparta Prague (1-4)
  Bayer 04 Leverkusen 0-0 Villarreal (0-2)
  Coutinho akinyoosha mikono angani kufurahia baada ya kuifungia bao muhimu la ugenini Liverpool Uwanja wa Old Trafford PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  LIVERPOOL imekwenda Robo Fainali ya michuano ya UEFA Europa League baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Manchester United usiku wa Alhamisi Uwanja wa Old Trafford.Manchester United walitangulia kwao bao la kwaju wa penalti la Anthony Martial dakika ya 32, kabla ya Philippe Coutinho kuisawazishia Liverpool dakika ya 45.
  Liverpool inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya awali kushinda 1-0 wiki iliyopita Uwanja wa Anfield.  
  Tottenham Hotspur nayo imeaga michuano hiyo baada ya kufungwa 2-1 na Borussia Dortmund Uwanja wa White Hart Lane, London. Mabao yote ya Dortmund yamefungwa na Mwanasoka Bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 24 na 70, wakati la Spurs limefungwa na Heung-Min Son dakika ya 73.
  Dortmund inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 Ujerumani. 
  Sevilla imeifunga 3-0 FC Basel, mabao ya Adil Rami na Kevin Gameiro mawili Uwanja wa Ramon-Sanchez Pizjuan, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya awali kutoa sare ya 0-0 ugenini.
  Mshambuliaji wa Dortmund, Pierre Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia timu yake dhidi ya Tottenham PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Shakhtar Donetsk imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya RSC Anderlecht, bao pekee la Eduardo Alves da Silva dakika za majeruhi Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion, hivyo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kushinda 3-0 nyumbani.
  Sporting Braga imeifunga 4-1 Fenerbahce, mabao ya Ahmed Hassan, Josue Filipe Soares Pesqueira,  Nikola Stojiljkovic na Rafael Alexandre Fernandes Ferreira Silva, huku la wageni likifungwa na Alper Potuk Uwanja wa Estadio Municipal de Braga.
  Valencia CF imeshinda 2-1 dhidi ya Athletic Club, mabao yake yakifungwa na Santiago Mina Lorenzo na Aritz Aduriz Zubeldia Uwanja wa Mestalla. Lakini ni Athletic Club, inayosonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya jumla ya 2-2, kufuaia kushinda 1-0 kwenye mchezo wa kwanza.
  Sparta Prague imelazimishwa sare ya 0-0 na Dully Sukes, wakati Bayer 04 Leverkusen imelazimishwa sare ya 0-0 na Villarreal BayArena
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAITUPA NJE MAN UNITED ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top