• HABARI MPYA

    Thursday, March 24, 2016

    MKWASA: MSIKOSE TAIFA JUMATATU YA PASAKA

    Na Prince Akbar, D’JAMENA
    KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa (pichani kushoto) amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi Jumatatu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuisapoti timu hiyo ikimenyana na Chad.
    Taifa Stars jana imeshinda 1-0 Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini D'jamena dhidi ya wenyeji, Chad katika mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, bao pekee la Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji.
    Na vikosi vyote, Chad na Tanzania vitapanda ndege moja leo kuelekea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa marudiano na wa kwanza wa mzunguko wa pili, utakaofanyika Jumatatu.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE mjini hapa baada ya mchezo wa jana, Mkwasa kwanza aliwapongeza vijana wake kwa kazi nzuri hadi kupata ushindi huo, licha ya kucheza kwenye mazingira magumu ya joto kali.
    Wachezaji wa Taifa Stars wakimpongeza Nahodha wao, Mbwana Samatta (10) baada ya kufunga
    Samatta (kushoto) akimhsukuru Farid Mussa (wa pili kulia) kwa kumpa krosi ya bao

    “Tulikuwa na dakika 90 ngumu sana, joto kali na jua pia, lakini tunamshukuru Mungu tumeshinda na sasa tunaelekeza akili zetu kwenye mchezo wa marudiano Jumatatu,”amesema.
    Ushindi wa jana unaifanya Tanzania ifikishe pointi nne baada ya mechi tatu, kufuatia kufungwa 3-0 awali na Misri mjini Cairo na kulazimishwa sare ya 0-0 na Nigeria Dar es Salaam mwaka jana.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA: MSIKOSE TAIFA JUMATATU YA PASAKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top