• HABARI MPYA

  Thursday, March 17, 2016

  TIKETI YANGA NA APR KUUZWA JUMAMOSI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIKETI za mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Yanga SC na APR ya Rwanda zitaanza kuuzwa siku ya mchezo, Jumamosi.
  Na kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa ni Sh. 5,000 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba kiingilio hicho kitakuwa ni kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
  Mashabiki wa Yanga watanunua tiketi za mechi baina ya timu yao na APR Jumamosi

  Muro amesema kwamba kwa ujumla eneo lote la mzunguko linalohusisha viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu watu wataketi kwa Sh. 5,000.
  Muro amesema VIP A tiketi yake itanunuliwa kwa Sh. 25,000, wakati VIP B  na C kote kila tiketi itauzwa Sh. 20,000.
  Amesema tiketi zitaanza kuuzwa mapema siku ya mchezo, Jumamosi katika maeneo ya siku zote, ikiwemo Uwanja wa karume na Uwanja wa Taifa. 
  Yanga itaingia katika mchezo wa Jumamosi ikiwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele, baada ya ushindi wa ugenini wa 2-1 Jumamosi iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIKETI YANGA NA APR KUUZWA JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top