• HABARI MPYA

  Thursday, March 17, 2016

  SIMBA YAMFUNGIA NA KUMVUA UNAHODHA ISIHAKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imemfungia kwa mwezi mmoja pamoja na kumvua Unahodha, beki wake wa kati chipukizi, Hassan Isihaka (pichani kulia) baada ya kukutwa na hatia ya utovu wa nidhamu.
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Manara amewaambia Waandisji wa Habari leo kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezaji huyo kukutwa na hatia ya kumtolea 'maneno machafu' kocha wa klabu, Mganda Jackson Mayanja.
  Manara amesema adhabu hiyo kwa Isihaka ambaye pia ni beki wa kati wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni onyo kwa wachezaji wengine wa klabu hiyo wasifikirie kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu katika timu.
  Isihaka anadaiwa 'kumjibu utumbo' kocha Mayanja kabla ya mechi ya jana ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Singida United Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwezi uliopita.
  Inadaiwa Isihaka alimtukana Mayanja kwenye chumba cha kubadilishia nguo Uwanja wa Taifa kabla ya mchezo huo wa michuano ya Kombe la Azam Sports Federation ambao SImba ilishinda 5-1. 
  Siku moja baada ya kudaiwa kufanya kitendo hicho, Isihaka alisimamishwa kwa muda usiojulikana kabla ya mchezaji huyo kuomba radhi siku mbili baadaye.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA YAMFUNGIA NA KUMVUA UNAHODHA ISIHAKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top