• HABARI MPYA

  Thursday, March 17, 2016

  OKWI AREJESHWA KIKOSINI UGANDA

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uganda, The Cranes baada ya karibu nusu mwaka.
  Kocha Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’ amemuorodhesha Okwi anayechezea Sondyerske ya Denmark katika kikosi chake cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya mechi mbili dhidi ya Burkina Faso za Kundi D kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani.
  Katika taarifa yake kwa BIN ZUBEIRY SPORTS – SPORTS ONLINE leo, Micho pia amewaita wachezaji wawili wa Simba, beki Juuko Murshid na mshambuliaji Hamisi Kiiza.
  Watu wa kazi; Emmanuel Okwi (kulia) na Hamisi Kiiza (kushoto) woyte wameitwa The Cranes
  Micho aliamua kuachana na Okwi baada ya kiwango chake kushuka, lakini sasa mchezaji huyo wa zamani wa Yanga pia ameimarika na anafanya vizuri Ligi Kuu ya Denmark.
  Uganda watakuwa wageni wa Burkina Faso Ijumaa ijayo mjini Ouagadougu kabla ya timu hizo kurudiana siku tatu baadaye mjini Kampala, Uganda. 
  Uganda inaongoza Kundi D kwa pointi zake sita baada ya kuzifunga Comoro na Botswana katika mechi za awali mwaka jana, ikifuatiwa na Burkina Faso yenye pointi tatu sawa na Botswana, wakati Comoro inashika mkia ikiwa haina pointi.  
  Kikosi kamili cha wali alichoita Micho kinaundwa na makipa; Onyango Denis (Mamelodi Sundowns, Afrika Kusini), Odonkara Robert (Saint George, Ethiopia), Jamal Salim (El Merreikh, Sudan), Alitho James (Vipers).
  Mabeki; Iguma Denis (Al Ahed, Lebanon), Nsubuga Joseph (Bright Stars), Okoth Denis (KCCA), Ochaya Joseph (KCCA), Muleme Isaac (SC Villa), Juuko Murushid (Simba, Tanzania), Isinde Isaac (Saint George, Ethiopia), Waswa Hassan Mawanda (Al Shorta, Iraq), Awanyi Timothy (KCCA), Muwanga Bernard (Bright Stars).
  Viungo; Aucho Khalid (Gor Mahia, Kenya), Mawejje Tony (Thottur, Iceland), Azira Mike (Colorado Rapids, Marekani), Ntege Ivan (KCCA), Mugerwa Yassar (Orlando Pirates, Afrika Kusini), Oloya Moses (Binh Duong, Vietnam), Serumagga Mike (SC Villa), Miya Farouk (Standard Liege, Ubelgiji), Kizito Luwagga Wiliam (CD Feirense, Ureno), Walusimbi Godfrey (Gor Mahia, Kenya). 
  Washambuliaji; Massa Geoffrey (Bloemfontein Celtics, Afrika Kusini) Okwi Emanuel (Sondyerske, Denmark), Hamisi Kiiza (Simba, Tanzania), Sekisambu Erisa (Vipers), Okhuti Ceasar (KCCA) na Lubega Edrisa (Proline).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AREJESHWA KIKOSINI UGANDA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top