• HABARI MPYA

  Wednesday, March 16, 2016

  NDUGU WA KIPRE WAPEWA STARS NA CHAD

  MAREFA wa Ivory Coast, nchi wanayotoka wachezaji wa Azam, Serge Wawa, Kipre Tchetche na Kipre Baluo, watachezesha mechi ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani kati ya wenyeji, Chad na Tanzania Ijumaa ijayo.
  Hao ni Jean-Jacques Ndala Ngambo atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Olivier Safari Kabene na Nabina Blaise Sebutu watakaoshika vibendera pembezoni mwa Uwanja wa Idriss Mahamat Ouya mjini N'Djamena.
  Taifa Stars itamenyana na Chad mara mbili mfululizo wiki ijayo nyumbani na ugenini  

  Tanzania inashika nafasi ya tatu katika Kundi G ikiwa na pointi moja baada ya kufungwa 3-0 na Misri mjini Cairo na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria Dar es Salaam mwaka jana, wakati Chad haina pointi baada ya kufungwa na Super Eagles na Mafarao katika mechi za mwanzo. 
  Misri ndiyo inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi nne na timu hizo pia zitamenyana baina yao wiki ijayo nyumbani na ugenini.   
  Mchezo wa marudiano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Tanzania na Chad utachezeshwa na marefa wa Djibouti Machi 28.
  Hao ni Djamal Aden Abdi atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera, Abdillahi Mahamoud Iltireh na Farhan Bogoreh Salime.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NDUGU WA KIPRE WAPEWA STARS NA CHAD Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top