• HABARI MPYA

    Wednesday, March 16, 2016

    NIYO, MIGI WOTE WAITWA AMAVUBI KWA AFCON

    VIUNGO nyota wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Jean Baptiste Mugiraneza wa Azam FC na Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima wote wameitwa kwenye kikosi cha Rwanda kwa ajili ya michezo miwili ya Kundi H kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Mauritius wiki ijayo.
    Kocha Muingereza, Jon McKinstry amechukua wachezaji 15 wa kikosi kilichofika Robo Fainali ya michuano ya CHAN mapema mwaka huu mjini Kigali kati ya 26 alioita katika kikosi chake cha awali.
    Rwanda itamenyana na Mauritius Jumamosi ya Machi 26 mjini Belle-Vue kabla ya kurudiana siku tatu baadaye mjini Kigali na Amavubi inatarajiwa kuingia kambini Jumamosi ya Machi 19 kuanza maandalizi ya mechi hiyo.
    Haruna Niyonzima (kulia) na Jean Mugiraneza wote wameitwa Amavubi

    Rwanda ina pointi tatu sawa na Mauritius, wakizidiwa pointi tatu na vinara wa kundi hilo, Ghana wakati Msumbiji haina pointi na inashika mkia.
    Kikosi kamili cha Amavubi kinaundwa na makipa; Eric Ndayishimiye (Rayon Sports), Olivier Kwizera (APR), Marcel Nzarora (Police) na Andre Mazimpaka (Mukura VS).
    Mabeki; Michel Rusheshangoga (APR), Fitina Omborenga (SC Kiyovu), Celestin Ndayishimiye (Mukura VS), Abouba Sibomana (Gor Mahia, Kenya), Soter Kayumba (AS Kigali), Abdul Rwatubyaye (APR), Emery Bayisenge (APR) na Salomon Nirisarike (Sint-Truidense, Ubelgiji).
    Viungo; Yannick Mukunzi (APR), Djihad Bizimana (APR), Jean Baptiste Mugiraneza (Azam, Tanzania), Amran Nshimiyimana (Police), Haruna Niyonzima (Yanga SC, Tanzania), Dominique Savio Nshuti (Rayon Sports), Innocent Habyarimana (Police), Jean Claude Iranzi (APR), Yussufu Habimana (Mukura VS), Muhadjiri Hakizimana (Mukura VS)
    Washambuliaji; Ernest Sugira (AS Kigali), Quentin Rushenguziminega (Lausanne Sport, Uswisi), Elias Uzamukunda (Le Mans, Ufaransa) na Dany Usengimana (Police).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NIYO, MIGI WOTE WAITWA AMAVUBI KWA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top