• HABARI MPYA

  Wednesday, March 16, 2016

  YOUNG AREJEA MAN UNITED KUIVAA LIVERPOOL

  WACHEZAJI wawili majeruhi wa Manchester United, Ashley Young na Cameron Borthwick-Jackson wako fiti kuelekea mchezo wa kesho wa Europa League dhidi ya mahasimu, Liverpool baada ya kupona maumivu yao. 
  Young amerejea mazoezini baada ya miezi miwili ya kuwa nje na leo amefanya mazoezi wakati Manchester United ikijiandaa kwa mechi ya Europa League dhidi ya Liverpool Uwanjawa Old Trafford kesho usiku.
  WInga huyo wa England hajaonekana uwanjani tangu United iifunge Liverpool 1-0 Uwanja wa Anfield Januari 17 baada ya kwenda kufanyiwa upasuaji Marekani kutokana na matatizo ya nyonga. 

  Winga wa Manchester United, Ashley Young akitabasamu wakati wa mazoezi leo kujiandaa na mechi dhidi ya Liverpool PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Lakini haijajulikana kama Young atacheza kesho dhidi ya kikosi cha Jurgen Klopp baada ya kuwa nje kwa muda refu, lakini yuko vizuri. 
  Nahodha Wayne Rooney, Phil Jones, Luke Shaw na Will Keane sasa wanabaki kuwa wachezaji pekee majeruhi, baada ya Cameron Borthwick-Jackson pia kufanya mazoezi leo asubuhi Uwanja wa Carrington.
  Borthwick-Jackson hajacheza tangu United iifunge 3-0 Shrewsbury katika Kombe la FA February 22.
  Kikosi cha Louis van Gaal kilionekana kipo vizuri kuelekea mchezo huo ambao wanahitaji kukipiku kipigo cha 2-0 walichopewa wiki iliyopita Uwanja wa Anfield kwa mabao ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino ili kwenda Robo Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YOUNG AREJEA MAN UNITED KUIVAA LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top