• HABARI MPYA

    Friday, March 18, 2016

    YAYA AREJESHWA KIKOSINI IVORY COAST

    MKONGWE Yaya Toure atarejea katika soka ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya mwaka, kufuatia kuorodheshwa kwenye kikosi cha Ivory Coast kwa mechi mbili dhidi ya Sudan kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika wiki ijayo.
    Kiungo huyo wa Manchester City mwenye umri wa miaka 32, hajachezea Tembo wa Ivory Coast tangu awe Nahodha wa kikosi kilichotwaa taji la AFCON Februari mwaka jana, akikosa mechi za mwanzo za kufuzu fainali zijazo zitakazofanyika Gabon mwaka 2017 pamoja na mechi za awali za kufuzu Kombe la Dunia 2018.
    "Yaya Toure aliomba mapumziko, jambo ambalo lilieleweka. Ametoa mchango mkubwa kwenyetimu na tulitumaini kumpa mapumziko," amesema kocha Michel Dussuyer.

    Yaya Toure amerejeshwa katika kikosi cha Ivory Coast kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya mwaka 

    "Nafikiri ametumia muda huo vizuri kujipumzisha na kujipanga upya, kama kushinda taji la pili mfululizo la Mataifa ya Afrika na kujipanga kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya nne, ambayo itakuwa babu kubwa na kujiwekea rekodi mpya,".
    Max Gradel wa Bournemouth amerejea pia baada ya kupona maumivu akiorodheshwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 kwa ajili ya mechi hizo mbili, ya kwanza mjini Abidjan Machi 25 na Khartoum siku nne baadaye, wakati beki wa Sunderland, Lamine Kone, mchezaji wa zamani wa timu za vijana za Ufaransa ameitwa kwa mara ya kwanza.
    Kikosi kitamuhusisha pia beki wa pembeni wa Paris St Germain, Serge Aurier, ambaye alikuwa amesimamishwa na mabingwa hao wa Ufaransa mwezi uliopita kwa kumtukana kocha Laurent Blanc na wachezaji wenzake kadhaa kwenye video aliyoposti kwenye mtandao.
    Aurier amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha wachezaji wa cha PSG akiba tangu mwezi uliopita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YAYA AREJESHWA KIKOSINI IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top