• HABARI MPYA

    Friday, March 18, 2016

    LIVERPOOL WAPEWA DORTMUND YA AUBAMEYANG

    Mwanasoka Bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Borussia Dortmund dhidi ya Tottenham jana na kutinga Robo Fainali

    RATIBA YA ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE 

    Braga vs Shakhtar Donetsk
    Villarreal vs Sparta Prague
    Athletic Bilbao vs Sevilla
    Borussia Dortmund vs Liverpool
    (Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Aprili 7 na marudiano Aprili 14, mwaka huu)
    KOCHA Jurgen Klopp atakutana na timu yake ya zamani, orussia Dortmund baada ya Liverpool kupangiwa na wababe wa Ujerumani katika Robo Fainali ya Europa League leo.
    Mwalimu huyo wa Kijerumani aliachana na timu hiyo ya nyumbani kwao mwaka 2015 baada ya miaka saba ya kuwa kazini.
    Na aliondoka baada ya kuipa mataji mawili ya Bundesliga na kutwaa mataji mawili kwa mpigo mwaka 2012 kabla ya kuifikisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa ambako walifungwa na Bayern Munich.
    Mechi nyingine za Robo Fainali ni kati ya Braga na Shakhtar Donetsk, Villarreal na Sparta Prague na Athletic Bilbao na Sevilla.
    Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Aprili 7 na marudiano Aprili 14, mwaka huu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIVERPOOL WAPEWA DORTMUND YA AUBAMEYANG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top