• HABARI MPYA

  Friday, March 18, 2016

  BARCA NA ATLETICO MADRID ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Barcelona imeifunga mara zote mbili Atletico Madrid katika La Liga msimu huu, 2-1 kila mechi na mchezo wao unatarajiwa kuwa Robo Fainali tamu zaidi ya zote za Ligi ya Mabingwa mwaka huu.

  Nyota wa Barcelona, Leonel Messi akipasua katikati ya wachezaji wa Atletico Madrid Uwanja wa Vicente Calderon katika moja ya mechi zilizopita baina ya timu hizo

  ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 

  WOLFSBURG vs REAL MADRID
  BAYERN MUNICH vs BENFICA
  BARCELONA vs ATLETICO MADRID
  PSG vs MANCHESTER CITY
  (Mechi za kwanza Aprili 5 na 6 na marudiano Aprili 12 na 13, mwaka huu)
  MANCHESTER City ya England watamenyana na PSG ya Ufaransa katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya droo iliyopangwa leo.
  Mabingwa watetezi, Barcelona watamenyana na wapinzani wao wa la Liga, Atletico Madrid, wakati vigogo wengine wa Hispania, Real Madrid watamenyana na Wolfsburg ya Ujerumani.
  Bayern Munich ya Ujerumani watamenyana na Benfica Ureno katika Robo Fainali ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa mwaka huu.
  Barcelona imeifunga mara zote mbili Atletico Madrid katika La Liga msimu huu, 2-1 kila mechi na mchezo wao unatarajiwa kuwa Robo Fainali tamu zaidi ya zote za Ligi ya Mabingwa mwaka huu.
  Mechi za Robo Fainali zinatarajiwa kuchezwa Aprili 5 na 6, wakati marudiano yatakuwa Aprili 12 na 13. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCA NA ATLETICO MADRID ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top