• HABARI MPYA

  Thursday, March 17, 2016

  BAYERN YAKAMILISHA ZA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

  Mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski akienda hewani pembezoni mwa lango kuifungia timu yake katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Juventus katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Allianz Arena usiku wa Jumatano. 
  Bayern wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-4, kufuatia awali kutoa sare ya 2-2 Italia na sasa inaungana na Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid zote za Hispania, Manchester City ya England, OSG ya Ufaransa na Benfica ya Ureno kutinga Robo Fainali. 
  Katika mchezo huo uliodumu kwa dakika 120, mabao ya Bayern yamefungwa na Robert Lewandowski dakika ya 73, Thomas Muller dakika ya 91, Thiago Alcantara dakika ya 108 na Kingsley Coman dakika ya 110, wakati ya Juventus yamefungwa na Paul Pogba dakika ya tano na Juan Cuadrado dakika ya 28. PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BAYERN YAKAMILISHA ZA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top