• HABARI MPYA

    Saturday, April 18, 2026

    FOUNTAIN GATE YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 ARUSHA


    TIMU ya Fountain Gate FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
    Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na kiungo Henry David dakika ya 64 na beki wa kushoto, Mnigeria, Obinna Awara dakika ya 68 kwa penalti, wakati bao pekee la Mtibwa Sugar limefungwa na kiungo Nassor Kiziwa dakika ya 76.
    Kwa ushindi huo, Fountain Gate inafikisha pointi 19 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 13, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 23 nafasi ya tisa kwenye ligi ya timu 16 baada ya timu zote kucheza mechi 19.
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao. 
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-1 ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top