• HABARI MPYA

  Wednesday, February 13, 2019

  SAOURA WACHUNGULIA ROBO FAINALI BAADA YA KUIPIGA VITA 1-0

  TIMU ya JS Saoura imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) usiku wa jana Uwanja wa Agosti 20, 1955 mjini Bechar nchini Algeria. 
  Katika mchezo huo ambao mshambuliaji Mtanzania wa JS Saoura, Thomas Ulimwengu alikuwa benchi muda wote, bao hilo pekee limefungwa kiungo Muagleria Ziri Hammar dakika ya 78 ambaye alitumia vyema kabisa makosa ya walinzi wa AS Vita.
  Ikumbukwe mchezo wa kwanza baina ya timu hizo wiki iliyopita mjini Kinshasa, Vita ililazimishwa sare ya kufungana 2-2 na JS Saoura.

  Sasa Vita inashika mkia Kundi D kwa pointi zake nne, ikizidiwa pointi moja na JS Saoura, mbili na Simba SC ya Tanzania na tatu na Al Ahly ya Misri.
  Mechi zijazo, Saoura ataikaribisha Simba SC mjini Bechar na AS Vita wataikaribisha Al Ahly mjini Kinshasa Jumamosi ya Machi 9. 

  MATOKEO MECHI ZOTE ZA JANA LIGI                 YA MABINGWA AFRIKA

  FTEsperance2 - 0Orlando PiratesView eventsMore info
  FTSimba1 - 0Al AhlyView eventsMore info
  FTASEC Mimosas0 - 0Mamelodi SundownsMore info
  FTHoroya2 - 0PlatinumView

  More info
  FTClub Africain0 - 0TP MazembeMore info
  FTWydad Casablanca0 - 0Lobi StarsMore info
  FTSaoura1 - 0Vita Club
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAOURA WACHUNGULIA ROBO FAINALI BAADA YA KUIPIGA VITA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top