• HABARI MPYA

    Sunday, June 03, 2018

    WAPYA WARUHUSIWA SPORTPESA SUPER CUP, MICHUANO YAANZA LEO YANGA NA JKU ZAKATA UTEPE

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WAKATI michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza leo Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, waandaaji wameruhusu wachezaji wapya waliosajiliwa baada ya msimu kucheza.
    Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwa simu kutoka Nakuru kwamba wachezaji wapya wataruhusiwa kucheza.
    Michuano hiyo inashirikisha timu nane, nne za Kenya ambazo ni mabingwa watetezi, Gor Mahia FC, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz, tatu za Tanzania Bara, ambazo ni Yanga SC, Simba SC, Singida United FC na moja kutoka Zanzibar, JKU.
    Nahodha wa Yanga, Mzimbabwe Thabani Kamusoko akipokea jezi kutoka kwa Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya jana tayari kwa mchezo wa leo

    Yanga watafungua dimba kwa mchezo wa mchana na Kakamega Homeboyz, kabla ya mabingwa watetezi, Gor Mahia kumenyana na JKU.
    Simba SC watatupa mguu wao wa kwanza kesho kwa kumenyana na Kariobangi Sharks katika mchezo wa mchana, kabla ya Singida United kumenyana na AFC Leopards jioni.
    Washindi wa mechi hizo watakutana katika Nusu Fainali Juni 7, ya kwanza ikikutanisha washindi wa mechi za leo na ya pili ikikutanisha washindi wa mechi za kesho.
    Na fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Juni 10 na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England. 
    Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAPYA WARUHUSIWA SPORTPESA SUPER CUP, MICHUANO YAANZA LEO YANGA NA JKU ZAKATA UTEPE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top