• HABARI MPYA

  Sunday, June 03, 2018

  MTIBWA SUGAR NA SINGIDA UNITED KATIKA PICHA JANA ARUSHA

  Mshambuliaji wa Singida United, Mzimbabwe Tafadzwa Kutinyu akimiliki mpira katikati ya wachezaji wa Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) jana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha jana. Mtibwa Sugar ilishinda 3-2
  Kiungo wa Mtibwa Sugar, Salim Kihimbwa akigagaa chini baada ya kuangushwa na kiungo wa Singida United, Mudathir Yahya (kulia)
  Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Kevin Sabato akipambana katikati ya wachezaji wa Singida
  Kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga akimdhibiti beki wa Singida United, Shafiq Batambuze
  Salim Kihimbwa akipasua katikati ya wachezaji wa Mtibwa Sugar
  Beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Isihaka akiwa juu kupiga mpira dhidi ya mshambuliaji wa Singida United, Lubinda Mundia
  Kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph Shindika akipiga mpira kuondosha kwenye eneo la hatari 
  Winga wa Singida United, Deus Kaseke akiwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar
  Kikosi cha Singida United kabla ya mchezo wa jana 
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kabla ya mechi ya jana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR NA SINGIDA UNITED KATIKA PICHA JANA ARUSHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top