• HABARI MPYA

  Friday, June 01, 2018

  MAN UNITED MBIONI KUKAMILISHA USAJILI WA BEKI MRENO

  BEKI wa kulia, Diogo Dalot wiki ijayo anatarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya kuelekea kukamilisha uhamisho wake, Manchester United kutoka Porto.
  Dalot amekuwa akipatiwa matibabu ya goti lake wakati United ikiendelea na majadiliano ya uhamisho wake wa Pauni Milioni 17.4. 
  United inamtaka beki huyo wa kulia akashindane na Antonio Valencia, mwenye umri wa miaka 33 na anahitaji matibabu ya uhakika ya goti lake.
  Dalot ni mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Ureno chini ya umri wa miaka 21 ambaye anaweza pia kucheza beki ya kushoto. 

  Diogo Dalot anatarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo vya afya Manchester United wiki ijayo PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Alianza kuchezea kikosi cha kwanza cha Ureno Porto Februari mwaka huu katika nafasi hiyo na akacheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya timu hiyo ikitoka sare ya 0-0 na Liverpool. 
  Aliisaidia Ureno kushinda michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2016, akifunga mabao mawili kwenye mechi tano mjini Azerbaijan likiwemo moja la kwenye fainali dhidi ya Hispania.
  United inatarajiwa kukamilisha mpango wa kumuuza Matteo Darmian kwa Pauni Milioni 11.5 kwenda vigogo wa Serie A, Juventus.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED MBIONI KUKAMILISHA USAJILI WA BEKI MRENO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top