• HABARI MPYA

  Friday, June 01, 2018

  ABRAMOVICH AFIKIRIA KUITEMA CHELSEA BAADA YA MIZENGWE YA VISA

  MMILIKI wa Chelsea, Roman Abramovich leo amesitisha uwekezaji wa Pauni Bilioni 1 wa kuuendeleza Uwanja wa Stamford Bridge na kusitisha maombi yake ya visa ya kuingia Uingereza kutokana na vita baina ya Urusi na Uingereza juu ya sumu aliyowekwa jasusi mjini Salisbury. 
  Bilionea huyo Mrusi mwenye umri wa miaka 51, anafikiri kuomba uraia wa Israeli kutamuwezesha kupata tema nafasi ya kuingia ya England.
  Abramovich, mwenye utajiri wa Pauni Bilioni 9.3, inaelezwa ana mpango mzuri wa kuikuza Chelsea. 
  Lakini ugomvi wake na Uingereza umezidi kukuwa leo baada ya vyanzo kusema anataka kutoa maombi yake ya visa baada ya kuchoka kusubiri kwa muda mrefu.

  Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich anataka kuachana na timu hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  Abramovich ametakiwa kuthibitisha namna alivyopata utajiri wake ili aweze kupatiwa kupatiwa visa ya kuingia tena Uingereza.
  Hatua huyo inafuatia Serikali kuanzisha vita maalum ya kuchunguza namna watu wanavyitajirika na mfanyabiashara huyo wa Urusi, mmiliki wa klabu ya Chelsea FC amefungiwa rasmi kuingia Uingereza hadi hapo atakapoonyesha fedha zake ni safiu.
  Matajiri wengine wakubwa waliopo Uingereza pia wanachunguzwa juu ya namna walivyotajirika na pia wanavyoutumia utajiri wao.

  Roman Abramovich (kushoto) katika picha ya pamoja na Rais Vladimir Putin mwka 2016 PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Hiyo inafuatia kuibuka kwa mtafaruku baina na nchi hizo mbili, baada ya Uingereza kudai Urusi ilitupa watu wa kwenda kumuwekea sumu jasusi Sergei Skripal na na binti yake mjini Salisbury.
  Serikali ya Uingereza imeilaumu Urusi na Waziri Mkuu, Theresa May amesema tukio hilo ni kama 'kudharauliwa' na akafukuza wanadiplomasia kadhaa wa Kirusi nchini humo.
  Abramovich, ambaye yuko nje ya Uingereza na alikosa fainali ya Kombe la FA, timu yake, Chelsea ikishinda 1-0 dhidi ya Manchester United Jumamosi, anachukuliwa kama muombaji mpya wa visa ya kuingia nchini humo.
  Tayari Rais wa Urusi, Vladimir Putin ambaye ni swahiba wa Abramovich amekwishalalamikia namna Uingereza inavyomfanyia mfanyabiashara huyo, kwamba haimtendei haki.

  Abramovich aliinunua Chelsea mwaka 2003 kwa Pauni Milioni 60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABRAMOVICH AFIKIRIA KUITEMA CHELSEA BAADA YA MIZENGWE YA VISA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top