• HABARI MPYA

    Friday, June 01, 2018

    HERRERA MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA MWISHO WA MSIMU MAN U

    KIUNGO Ander Herrera ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa mwisho wa msimu wa 2017/2018 wa Manchester United kutokana na kura za mashabiki.
    Mspaniola huyo amepata ushindi wa kishindo kutokana na kupata asilimia 53 ya kura zilizopigwa kwenye mtandao wa ManUtd.com. 
    Herrera amewashinda wachezaji wenzake Ashley Young aliyepata asilimia 31 na Chris Smalling aliyepata asilimia 16 baada ya kuingia fainali.
    Hii ni mara ya kwanza kwa Herrera kushinda tuzo hiyo tangu Aprili mwaka 2017, mwezi ambao pia alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya Sir Matt Busby.

    Ander Herrera amekuwa Mchezaji Bora wa Mwezi wa mwisho wa msimu wa 2017/2018 wa Manchester United  

    ORODHA KAMILI YA WACHEZAJI BORA WA MWEZI KWA MSIMU WA 2017/18
    Agosti: Paul Pogba
    Septemba: Anthony Martial
    Octoba: Anthony Martial
    Novemba: Ashley Young
    Desemba: Jesse Lingard
    Januari: Anthony Martial
    Februari: David De Gea
    Machi: Romelu Lukaku
    Aprili: Paul Pogba
    Mei: Ander Herrera
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HERRERA MCHEZAJI BORA WA MWEZI WA MWISHO WA MSIMU MAN U Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top