• HABARI MPYA

  Sunday, April 08, 2018

  SAMATTA ASABABISHA PENALTI YA BAO LA USHINDI GENK YAIPIGA STANDARD LIEGE 1-0 UBELIGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana aliisaidia klabu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Standard Liege katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee la ushindi, mshambuliaji kinda wa umri wa miaka 23, Leandro Trossard kwa penalti dakika ya 49.
  Na penalti hiyo ilitolewa baada ya Samatta kuangushwa chini na beki wa Standard Liege, Sebastien Pocognoli katika harakati za kumalizia krosi ya kiungo kutoka Ukraine, Ruslan Malinovskyi. 
  Mbwana Samatta akimtoka beki wa Standard Liege, Konstantinos Laifis jana Uwanja wa Luminus Arena

  Samatta jana amecheza kwa dakika zote 90, hiyo ni mechi yake ya 81 tangu alipojiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). 
  Na katika mechi hizo, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mashindano yote.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Mata, Seck, Malinovskyi, Pozuelo/Wouters dk88, Ndongala/Buffalo dk82, Trossard/Writers dk91 na Samatta.
  Standard Liege; Ochoa, Agbo/Djenepo dk82, Cop/Carlinhos dk70, Emond, Carcela, Pocognoli, Marin, Fai, Edmilson, Luyindama na Laifis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ASABABISHA PENALTI YA BAO LA USHINDI GENK YAIPIGA STANDARD LIEGE 1-0 UBELIGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top