• HABARI MPYA

    Friday, April 20, 2018

    WENGER ATANGAZA KUONDOKA ARSENAL MWISHONI MWA MSIMU



    Hatimaye Arsene Wenger ametangaza kuondoka Arsenal baada ya miaka 22 ya kuwa kazini PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    MATAJI ALIYOTWAA ARSENE WENGER  

    Ligi Kuu England: 
    Kushinda (3) - 1997/98, 2001/02, 2003/04
    Nafasi ya pili (6) - 1998/99, 1999/00, 2000/01, 2002/03, 2004/05, 2015/16
    Kombe la FA:
    Winners (7) - 1997/98, 2001/02, 2002/03, 2004/05, 2013/14, 2014/15, 2016/17
    Nafasi ya Pili (1) - 2000/01
    Kombe la Ligi:
    Nafasi ya Pili (3) - 2006/07, 2010/11, 2017/18
    Ligi ya Mabingwa:
    Nafasi ya Pili (1) - 2005/06
    UEFA Cup:
    Ushindi wa Pili (1) - 1999/00
    Ngao ya Jamii:
    Kushinda (6) - 1998/99, 1999/2000, 2002/03, 2004/05, 2014/15, 2015/16
    Nafasi ya Pili (2) - 2003/04, 2005/06
    Kocha Bora wa Msimu Ligi Kuu England (3) - 1997/98, 2001/02, 2003/04
    Kocha Bora wa Chama cha Soka wa Mwaka (2) - 2001/02, 2003/04
    Kocha Bora wa BBC Sports Personality wa Mwaka (2) - 2002, 2004
    Kocha Bora wa Ligi Kuu England wa Mwezi (15)

    MFARANSA Arsene Wenger amesema atajiuzulu katika klabu ya Arsenal mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka 22 ya kuwa kocha wa klabu hiyo ya London.
    Babu huyo mwenye umri wa miaka 68, aliyejiunga na Arsenal akitokea Nagoya Grampus Eight ya Japan mwaka 1996, ameandika taarifa nzuri kwa mashabiki wa klabu hiyo akiwaambia juu ya kuondoka kwake, huku akiwaahidi upendo na sapoti daima.
    Wenger amesema hayo siku mbili tu kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya West Ham Jumapili mchana Uwanja wa Emirates, London. 
    Kumekuwa na shinikizo la kumtaka kocha huyo aondoke Emirates miaka ya karibuni kutokana na matokeo mabaya akishindwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya England tangu mwaka 2004. 
    Pamoja na hayo ameshinda mataji 10 makubwa na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London na ataendelea kukumbukwa kama kocha mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya Arsenal.
    Wenger amenukuliwa na tovuti ya Arsenal akisema; "Baada ya kutazama kwa umakini na majadiliano na klabu, nafikiri ni wakati mwafaka kwangu kung'atuka mwishoni mwa msimu. 
    "Ninajivunia kupewa kipaumbele cha kuitumikia klabu kwa miaka mingi ya kukumbukwa. Nimeongoza klabu kikamilifu na kwa kujitolea,"
    "Nataka kuwashukuru viongozi, wachezaji, Wakurugenzi na mashabiki ambao wameifanya hii klabu kuwa maalum. Nawaomba mashabiki kusimama nyuma ya timu ili tumalize msimu huu vizuri,"amesema. 
    Makocha wanaopewa nafasi ya kumrithi Wenger, pamoja na Nahodha wa zamani wa klabu, Patrick Vieira ni Wajerumani Thomas Tuchel mwenye umri wa miaka 44 ambaye amekuwa hana timu tangu aondoke Borussia Dortmund mwaka jana na Joachim Low, Wataliano Carlo Ancelotti, Massimiliano Allegri na Brendan Rodgers.
    Kwa sasa Arsenal inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England na ipo katika katika Nusu Fainali ya Europa League ambako itamenyana na Atletico Madrid.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WENGER ATANGAZA KUONDOKA ARSENAL MWISHONI MWA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top